Habari
Wafanyabiashara katika mipaka nchini kurasimisha Biashara zao ili watambulike katika mifumo ya kibiashara.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Mb) amewaomba wafanyabiashara katika mipaka nchini kurasimisha Biashara zao ili watambulike katika mifumo ya kibiashara.
Mhe.Kigahe ameyasema hayo leo 20 Septemba 2024 wakati akizingumza na wafanayakazi wa kituo Cha forodha cha Holili kilichopo Wilaya ya Rombo Mkoa wa Kilimanjaro.
wafanyabiashara kurasimisha Biashara zao ili watambulike katika mifumo ya Serikali ili wafanye Biashara yao kwa uhakika mwisho wa siku Serikali ipate sehemu ya mapato yake hata kama ni kidogo kidogo.
Kigahe ,Amesema kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha wafanyabiashara wanatambulika katika mifumo rasmi ya kufanya Biashara utakaosaidia kutosumbulia pia waweze kuchangia pato la Taifa kwa kulipa kodi kama Sheria zinavyotaka.
Aidha Mhe . Kigahe amebainisha kuwa Serikali inafanya mpango wa kuongeza mipaka mingine rasmi ili kupunguza Biashara ya magendo inayofanyika hivi sasa inayochangia kuingiza Biashara zisizo na viwango na na zisizolipia Kodi.
Naye Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Forodha Bw.Mohamed Fukwa ameeleza Bidhaa zinazopita mara kwa mara kutoka bandari ya Mombasa kuelekea nchi jirani kupitia mpaka wa Holili ni Nguo (clothes)Mafuta Ghafi (Crude Palm Oil),Sukari (Brown Sugar),Viatu (shoes),Bidhaa Mchanganyiko (Assorted items),Chupa tupu (Empty Bottle),Vipuri (Auto spare parts),Mafuta ya msingi (Base Oil), Ethyl Alcohol,Pvc Resin na nk