Habari
Wafanyabiashara wahimizwa kuchangamkia fursa AfCFTA

Mkurugenzi wa Idara ya Viwanda, Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Lugano awahimiza wafanyabiashara kuchangamkia fursa adhimu eneo la soko huru la Biashara Afica - African Con betinental Free Trade Area (AfCFTA) ili kuongeza uzalishaji na uongezaji wa thamani kwenye mazao,mifugo na uvuvi.
Dkt Lugano ameyasema hayo leo tarehe 13 April,2023 katika ukumbi wa hoteli ya Dodoma wakati akitoa mada kwenye ufunguzi wa kongamano la wadau wa sekta ya kilimo kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah.
Kongamano hilo la tisa kufnyika linahusisha wadau wa sekta ya kilimo ili kufanya tathimini ya matokeo ya tafiti na maboresho ya sera,kanuni na sheria katika sekta ya kilimo ili kuweka mazingira wezeshi yatakayoleta mageuzi katika sekta ya kilimo na mnyororo wa thamani pindi utekelezaji wake utakapoanza.
Aidha akizungumza katika kongamano hilo Dkt. Lugano amewaomba wafanyabiashara waliotayari kufanya biashara katika eneo la soko huru la Biashara Africa -African Continental free Trade Area (AfCFTA) kubisha hodi kati Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara kwa lengo kukuza uchumi wa nchi na uchumi wa wafanyabishara wetu.
“Katika kujipanga serikali kwa sasa inaendelea kukamilisha mkakati wa kitaifa wa utekelezaji wa mkataba wa AfCFTA, wataalam wa wizara wapo Dar es Salaam wakishirikiana na sekta binafsi kwa lengo la kuweka mikakati bora na endelevu ya kuwezesha nchi yetu amesema” Dkt Lugano.
Kwa hiyo tunategemea kwamba mapendekezo yatakayotolewa katika mkutano huo yatakuwa na tija , kubwa hivyo tuwaombe wadau wa biashara waliotayari kufanya biashara chini ya AfCFTA wasisite kutuona ili tuweze kuwaunganisha katika programu zinazoendea
Aidha Dkt. Lugano ameongeza kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi saba ambazo zimeridhia mkataba huo na kuwa miongoni mwa nchi za awali ambazo zitanufaika kupitia program iliyoanzishwa na sekretarieti ya AFCFTA .