Habari
Waziri Kijaji akutana na kuongea na Wafanyabiashara na madereva wa malori mpakani Namanga - Arusha

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji.(Mb.) leo Mei 28, 202 amefanya ziara katika Kituo cha pamoja cha mpakani Namanga (OSBP) ilikujionea utendaji kazi wa taasisi mbalimbali zinazotoa huduma kwa wafanyabiasha pamoja na kuongea na madereva na wakala wa forodha na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili ili kuwawezesha kufanya biashara zao kwa urahisi.