Habari
Waziri Kijaji : Ametembelea Bandari ya Tanga na kujionea shughuli za upanuzi wa bandari

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa Mhe. Adam Malima Mei 30, 2022 ametembelea Bandari ya Tanga na kujionea shughuli za upanuzi wa bandari hiyo unavyoendelea ili kuiwezesha kupokea meli za mizigo kubwa na kuwa na uwezo wa kuhifadhi mizigo mingi kwa wakati mmoja. Hii ni hatua ya Serikali katika kuweka mazinhira bora na wezeshi kwa wafanyabiashara na wawekezaji.