Habari
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Shaban Omary amesema ushirikiano baina ya Tanzania na China unawezesha utekelezaji wa Sera ya Uchumi wa buluu na utalii

Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Mhe. Shaban Omary amesema ushirikiano baina ya Tanzania na China unawezesha utekelezaji wa Sera ya Uchumi wa buluu na utalii ambao unahusisha usafirishaji wa Mazao ya Bahari na Samaki.
Aidha amewashauri Watanzania wote nchini kufika katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba kujionea na kutumia fursa mbalimbali zilizopo ndani ya nchi na zile zilizopo nchini China.
Waziri Shaban ameyasema hayo Julai 4, 2023 katika hafla ya siku ya China (CHINA DAY) iliyofanyika kama programu moja wapo ya Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yaliyoanza Juni 28 hadi Julai 13, 2023 katika Viwanja vya Mwl. J. K.Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri Shaban pia amesema kutokana na ushirikiano huo baadhi ya makampuni kutoka China yameanza kutengeneza vyumba vya kuhifadhia bidhaa (COLD ROOM) ili kurahisisha usafirishaji wa Mazao ya Bahari na Samaki na kukuza uchumi wa bluu
Naye, Naibu Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesena Wachina ni washirika wakubwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo nq maadhimisho haya ya Sabasaba na ujenzi wa eneo la biashara la Ubungo(Ubungo bus terminal zamani)litakalo kuwa na Malls nyingi katika eneo hilo
Naye Balozi wa Jamhuri ya China Bi. Chen Mingjian amesema maadhimisho hayo yameendeleza mahusiano mazuri yakibiashara na kitamaduni kati ya Tanzania na China na Africa.