Habari
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ameshiriki katika Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji (wa kwanza kushoto) ameshiriki katika Mkutano wa 15 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Fedha na Uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika leo tarehe 12/5/2023 jijini Arusha.
Mkutano huo pamoja na mambo mengine umejadili masuala ya kibajeti ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.