Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara ashiriki Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika


Mheshimiwa Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu K. Kijaji (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika mara baada ya ufunguzi wa Kongamano la Africa CEO Forum linalofanyika katika Hoteli ya Sofitel Jijini Abidjan nchini Ivory Coast kuanzia tarehe 13 hadi 14 Juni, 2022.

Mheshimiwa Waziri amemuwakilisha Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano huo ambaye alipokea Mwaliko kutoka wa Rais wa Ivory Coast Mheshimiwa Alassane Ouattara.

Mkutano huo umehudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Nchi mbalimbali za Afrika akiwemo Rais wa Ivory Coast,  Rais wa Ghana, Makamu wa Rais wa Nigeria, n.k.