Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amewaahidi wafanyabiashara wa soko la mchele la Magugu mkoani Manyara kufanyia kazi   kero ya utozaji wa ushuru


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amewaahidi wafanyabiashara wa soko la mchele la Magugu mkoani Manyara kufanyia kazi 
 kero ya utozaji wa ushuru wa Shilingi 1500 kwa mfuko wa ujazo wa kilo 50  na kwa kushirikiana na Waziri wa Kilimo pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi.

Waziri Kijaji  ametoa ahadi hiyo Mei 12, 2023  alipotembelea soko la mchele la Magugu mkoani Manyara na kukutana na Wafanyabiashara kwa lengo la kujionea hali ya biashara katika soko hilo wakati wa mwanzo wa msimu wa mavuno ya Mpunga kwa mwaka 2023. 

Wakiongea na Waziri Kijaji, Wafanyabiashara wa Magugu wameipongeza Serikali kwa kusaidia kuboresha mazingira ya Wafabyabiashara wadogo na wameiomba Serikali iwapunguzie tozo ya ushuru wa Shilingi 1500 kwa mfuko wa ujazo wa kilo 50 kwa kuwa inaongeza gharama katika biashara.