Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu K. Kijaji (Mb.) amehutubia Kongamano la Uhamasishaji Biashara na Uwekezaji baina ya nchi za Afrika na Jiji la Loudi, Jimbo la Hunan, China


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu K. Kijaji (Mb.) amehutubia Kongamano la Uhamasishaji Biashara na Uwekezaji baina ya nchi za Afrika na Jiji la Loudi, Jimbo la Hunan, China hususani kwenye maeneo ya teknolojia ya Kilimo pamoja na utengenezaji wa vifaa mbalimbali vya maofisini. Kongamano hilo limefanyika Julai 1, 2023 jijini Changsha, China.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.),  Julai 1, 2023 ametembelea banda la  Tanzania katika Maonesho ya tatu baina ya China na Afrika ambayo yalianza tarehe 29 Juni, 2023. Maonesho hayo yanafanyika jijini Changsha, China.

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu K. Kijaji (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Bi. Rossella Lyu, Mkurugenzi wa Kampuni ya Greenchain ambayo imeonesha nia ya kununua maparichichi kutoka Tanzania na pia anataka kuwekeza kwenye uongezaji wa thamani wa zao la parachichi hasa kujenga kiwanda cha kukamua mafuta ya Parachichi. 

Pia Mkurugenzi huyo amesema anahitaji kuwekeza Tanzania kwenye maghala ya kuhifadhia matunda pamoja na mbogamboga ambazo zinatarajiwa kusafirishwa kwenda nje ya nchi. 

Aidha, Dkt. Kijaji amemuhakikishia mwekezaji huyo utayari wa Tanzania kufanya nae kazi ikiwemo kuhakikisha uwekezaji huo unafanyika nchini. 

Mazungumzo hayo yameshuhudiwa pia na Balozi Mbelwa Kairuki, Balozi wa Tanzania nchini China. Mazungumzo hayo yamefanyila Julai 1, 2023 jijini Changsha, China.