Habari
Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Ashatu Kijaji amekutana na Mkurungenzi mtendaji wa makampuni ya KEDA.

Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa makampuni ya KEDA Bw. Bryan
Kikao hicho kimefanyika tarehe 25 Mei 2023 katika ofisi ya Mhe Waziri jijini Dodoma. Aidha kikao hicho baina ya Mhe. Waziri na Mkurugenzi wa Makampuni ya KEDA kimefanyika kikiwa na lengo la kupokea taarifa ya hatua iliyofikiwa kuhusu ujenzi wa kiwanda cha Vioo vya Alminium kinachojengwa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani.