Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mkuu wa masuala ya Ushirika Duniani kutoka Newyork


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mkuu wa masuala ya Ushirika Duniani kutoka Newyork Bw. John Blood ambaye amefika nchini Tanzania na kupokelewa na uongozi wa kiwanda cha Vinywaji cha Tanzania (Tanzania Breweries Plc.).

Lengo la ziara ya Afisa Mkuu masuala ya Ushirika Duniani ni kuona fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania na maendeleo ya kiuchumi na pia mazungumzo yamelenga uzinduzi wa uwekezaji wa kiwanda kipya cha kuchakatua shahiri kilichopo Mkoani Kilimanjaro.