Habari
Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda Mount Meru Millers Ltd.

Waziri wa Uwekezaji Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha kukamua mafuta ya Alizeth cha Mount Meru Millers Ltd. Bw. Anil Zacharia (kushoto). Kiwanda hicho kipo kijiji cha Manguanjuki Mkoani Singida.
Lengo mazungumzo hayo ni kujadili mikakati kuelekea msimu wa uvunaji wa Alizeth ili kuhakikisha wakulima wananufaika na soko la zao hilo kupitia Viwanda vya ndani.