Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika ufunguzi wa Jukwaa la Pili la Baraza la Mawaziri wa Biashara wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA)


Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.), ameongoza ujumbe wa Tanzania katika ufunguzi wa Jukwaa la Pili la Baraza la Mawaziri wa Biashara wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) uliofunguliwa leo  tarehe 29/5/2023 na  Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto. 

Viongozi wengine waliohudhuria ufunguzi huo ni pamoja na Mhe. Azali Assoumani, Rais wa Muungano wa Comoro na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika pamoja na Mhe. Issouf Mahamadou, Rais Mstaafu wa Niger. 

Jukwaa la Mawaziri litafanyika kwa siku mbili na litafuatiwa na Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Biashara wa AfCFTA unaotarajiwa kufanyika tarehe 31/5/2023. 

Pamoja na masuala mengine Mkutano wa Mawaziri utajadili masuala ya Uasili wa Biadhaa wa Nguo na Mavazi pamoja na Magari.