Habari
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akikagua Trekta aina ya URSUS likilima shamba la Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Mkoani Morogoro

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), akikagua Trekta aina ya URSUS likilima shamba la Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Mkoani Morogoro tarehe 15 Septemba, 2023. Chuo cha SUA kilinunua matrekta ya URSUS 10 kutoka Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) kwa lengo la kutoa mafunzo ya kilimo kwa wanafunzi katika Chuo hicho. Matrekta yote 10 yanafanya kazi hadi sasa. Chuo cha SUA kina Wataalamu wenye uwezo wa kutoa mafunzo ya kiufundi na kufanya matengenezo ya nyenzo zote za kilimo, yakiwemo matrekta.