Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekitaka  Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro kuongeza uzalishaji wa bidhaa


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekitaka  Kiwanda cha Bidhaa za Ngozi cha Kilimanjaro kuongeza uzalishaji wa bidhaa ili ziweze kukudhi mahitaji ya soko la ndani na soko la nje.

Waziri Kijaji ameyasema  hayo Agosti 2, 2023 alipotembelea Kiwanda hicho kilichopo Mkoani Kilimanjaro kwa lengo la kujionea shughuli za uzalishaji na kitatua changamoto zilipo kiwandani hapo.

Aidha, Dkt Kijaji amesema bidhaa hizo kama Viatu, mabegi na mapochi  zinazotengenezwa na Kiwanda hicho kwa kitumia malighafi za ndani ya nchi zina asilimia 100  ya kukishi vigezo vya kuingia katika soko la eneo huru la biashara Afrika (AfCFTA).