Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekitaka Kiwanda cha Kuzalisha Bidhaa za Kibaolojia Tanzania (TBPL)


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekitaka Kiwanda cha Kuzalisha Bidhaa za Kibaolojia Tanzania (TBPL) kuzalisha kibiashara viuatilifu hai (Biopesticides) kwa kasi kwa ajili ya kupambana na wadudu waharibifu katika mazao ya kilimo wakati wa msimu wa mvua ujao.

Ameyasema hayo Septemba 21, 2023 akiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Lugano Wilson wakati wa Mkutano na Waansishi wa Habari kuhusu maendeleo ya Kiwanda cha Kuzalisha Bidhaa za Kibaolojia Tanzania (TBPL) uliofanyika kiwandani hapo, Kibaha mkoani Pwani.

Aidha, Amesema Wizara yake kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) imepanga kuunganisha utekelezaji wa Mradi wa BBT na bidhaa zinazozalishwa na TBPL hususani viatolifu hai visivyo na kemikali vilivyopata ithibati ili kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa na Programu hiyo katika soko la ndani na nje ya nchi.

Dkt Kijaji amabainisha kiwa viatilifu hai vilivyofanyiwa majaribio na kithibitishwa na TARI na kupatiwa cheti cha usajili na Mamlaka ya Udhibiti wa Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA) ni rafiki kwa watumiaji na mazingira, vinaongeza thamani ya mazao katika soko na ni chanzo cha soko la wageni.

Dkt. kijaji pia amesema kuwa Kiwanda hicho kimefanikiwa kuuza lita 272,444 za dawa ya viuadudu katika nchi 7 za Afrika ambazo ni Kenya, Angola, Niger, Botswana, Namibia, Eswatini na Msumbiji na ni bidhaa ya tano katika bidhaa 10 zinazotarajiwa kuuzwa katika soko la Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).

Aidha, Ameelezea kuwa Wizara yake kupitia Shirika lake la NDC, TAMISEMI, Wizara ya Afya na Wizara ya Fedha ziko katika hatua za mwisho za kuhuisha Mkataba wa ununuzi wa dawa za viuadudu vinavyozalishwa na TBPL ili kutimiza lengo la Serikali katika kutokomeza ugonjwa wa malaria nchini.

Naye, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) Dkt Nicholaus Shombe amesema Kiwanda cha kipekee Barani Afrika kina uwezo wa kuzalisha lita milioni 6 za bidhaa za kibailojia zisizo na kemikali kwa mwaka ikiwemo viuadudu vya kuua viluwiluwi wa mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria na magonjwa mengine yanayoambukizwa na mbu, viatilifu hai vya kuua wadudu waharibifu kwenye mazao na mbolea hai.