Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania kuendeleza uhusiano wa kibiashara na China


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji(Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza uhusiano wa kibiashara na China hususan katika uchakataji wa mazao ya kilimo na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2023. Tanzania inasafirisha mazao ya kilimo kama parachichi, kahawa, mahindi , ufuta na asali kwenda China.