Habari
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji(Mb.) amesema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji(Mb.) amesema Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini ili kuiwezesha sekta binafsi kuongeza uzalishaji zaidi.
Waziri Kijaji ameyasema hayo Septemba 13, 2023 akiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Dkt. Lugano Wilson alipokutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Bw. Obinna Anyalebeche, ujumbe wake katika Ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam.
Aidha, amekipongeza Kiwanda hicho kwa kuendelea kuongeza uzalishaji wa bidhaa kupitia viwanda vyao vilivyopo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Kilimanjaro.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni SBL Bw. Obinna Anyalebeche ameishukuru Serikali kwa kuendelea kiilea sekta binafsi ili kuhakikisha wanazalisha zaidi na kulipa kodi stahiki kwa Serikali.
Aidha, Bw. Anyalebeche ameanisha mpango wa kiwanda hicho kuhakikisha wanapata malighafi hapa nchini na kuwahakikishia wakulima soko katika mazao yanayohitajika kuzalisha bidhaa zao
See translation