Habari
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) ameshuhudia kuagwa kwa kundi la kwanza la asali ya Tanzania kabla ya kusafirishwa kwenda China.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) ameshuhudia kuagwa kwa kundi la kwanza la asali ya Tanzania kabla ya kusafirishwa kwenda China.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi iliyofanyika Desemba 25,2024 Jijini Dar es Salaam Dkt. Jafo amesema Usafirishaji wa asali hiyo unaanza kufungua fursa za masoko ya asali nje ya nchi hivyo ni Wakati sasa kwa Tanzania kujiandaa na kuchangamkia fursa za Masoko ya asali nchini China na kwingineko.
Dkt. Jafo pia amesema tukio hilo si la kusafirisha asali tu bali linaashiria kutimiza maono ya ukuaji wa uchumi na ushirikiano wa kimataifa na kutoa pongezi kwab China kwa imani yao ya kuanza kusafirisha na kutumia bidhaa za asali inayotoka Tanzania.
Aidha amesema Serikali inendelea kuweka mazingira wezeshi,pamoja na kuwekeza katika miundombinu ili krahisisha upatikanaji wa bidhaa za asali kwa wingi nchini.
Pia Dkt.Jafo amesema Tani 10 za asali zinayotarajiwa kusafirishwa kwenda China kwa majribio zikiwa na thamani ya zaidi Milioni 100 za Kitanznia.