Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

WANAWAKE WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2026 WILAYANI KONGWA


Wanawake wa Wizara ya Viwanda na Biashara wameungana na wanawake wote duniani kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2026 Wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Maadhimisho ya mwaka 2026 yanaongozwa na kauli mbiu isemayo: "Haki kwa Wanawake na Wasichana: Msingi wa Maendeleo Jumuishi kuelekea Dira ya Taifa 2050"

Kwa umoja na mshikamano mkubwa, wanawake hao
wamekusanyika kusherehekea na kutambua mchango wa wanawake katika maendeleo ya sekta ya Viwanda na Biashara na Taifa kwa ujumla.

Aidha, wanawake wameonesha dhamira ya kuendelea kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa kizazi chenye usawa, maendeleo na ustawi.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani hutoa fursa ya kuenzi juhudi, mafanikio na mchango wa wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo, pamoja na kuhamasisha jamii kuendelea kuunga mkono usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake katika maeneo ya kazi na jamii kwa ujumla.

Katika maadhimisho hayo, mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule.