Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Kamishina Jenerali wa World Expo Osaka 2025


Kamishina Jenerali wa World Expo Osaka 2025 kwa Tanzania na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Bi. Latifa Khamis amesema kongamano hilo ambalo ni sehemu ya ushiriki wa Tanzania katika maonesho ya World Expo Osaka 2025 linalenga kuwakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na Japan.

Ameysema hayo Mei 26, 2025 baada ya ufunguzi wa Kongamano la Biashara, Uwekezaji na Utalii lililofunguliwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ambalo lililowakutanisha wafanyabiashara wa Tanzania na wafanyabiashara na wawekezaji wa Japan katika ukumbi wa mikutano wa Hoteli ya Westin, Osaka, Japan ikiwa ni sehemu ya ushiriki wa Tanzania katika maonersho ya World Expo Osaka 2025

Mkurugenzi huyo alisema maeneo ambayo yamepewa kipaumbele katika kongamano hilo ni kwenye sekta ya nishati, madini, kilimo, huduma za kibenki, utalii, uwekezaji, afya ambapo wafanyabiashara wa Tanzania wanakutana na wafanyabiashara wa Japan kujadiliana namna ya kushirikiana katika kukuza biashara na uwekezaji.