Habari
Ziara ya Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mkoani Njombe

Ziara ya Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji: Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji ameanza ziara ya siku tano kutembelea mikoa ya Njombe, Mtwara na Lindi ambapo ziara yake imeanzia Mkoa wa Njombe leo tarehe 1 Machi, 2018. katika ziara hiyo Mhe. Mwijage anatembea kuona jitihada zilizofanywa katika uendelezwaji wa Viwanda, kukabidhi maeneo kwa mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya Viwanda, kutembelea ofisi za wakala wa Vipimo, Kutembelea Viwanda na kuzungumza na wafanyabiashara kutatua changamoto zao.