Kongamano la AfCFTA la Wanawake katika Biashara 2023. 6 - 8/12/2023 Dar es Salaam, Tanzania
Wafanyakazi wakiendelea na shughuli za uzalishaji wa nguo katika Kiwanda cha Took Garmet kilichopo Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uwekezaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA), Ubungo External, Dar es salaam.
Wafanyakazi wakiwa kazini katika Kiwanda cha nguo cha A to Z kilichopo Arusha kinachozalisha vyandarua vyenye dawa ya kuua wadudu
Wafanyakazi wakiendelea na kazi ya ushonaji katika Kiwanda cha kutengeneza nguo na mavazi cha A To Z kilichopo Mkoani Arusha
Wafanyakazi wakiwa kazini katika Kiwanda cha kutengeneza Vifaa vya Umeme cha Elsewedy Electric East Africa LTD kilichopo Kisarawe II Kigamboni, Jijini Dar es Salaam
Uzalishaji dawa za maji tiba (Fluid Therapy) mbalimbali katika Kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industry Limited kilichopo Mkoa wa Pwani.
Wafanyakazi wakipaki dawa katika vifungashio katika kiwanda cha Prince Pharmaceutical kilichopo jijini Mwanza. Kiwanda hiki ni moja ya juhudi za kuongeza uzalishaji wa dawa nchini na kukuza uchumi wa nchi
Mfanyakazi akishona kiatu katika Kiwanda cha Kilimanjaro International Leather Industries kinachojihusisha na uzalishaji wa bidhaa za ngozi. Kiwanda hicho kinamilikiwa na ubia kati ya Jeshi la Magereza na PSSSF na kipo katika Mkoa wa Kilimanjaro
Utengenezaji wa vifaa vya ujenzi katika kiwanda cha Kahama Oil Mills (KOM) kilichopo mkoani Shinyanga kilichofanya upanuzi kutoka Kiwanda cha uchakataji wa mbegu za Pamba ili kuzalisha mafuta na kuanza uzalishaji wa bidhaa za Mabati, plastiki na chuma.
Uzalishaji wa nguo zinazotokana na pamba katika Kiwanda cha “Sunflag Tanzania Ltd” kilichopo jijini Arusha. Kiwanda hiki hutumia pamba inayozalishwa hapa nchini.